Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (ABNA)- Kiongozi wa upinzani wa Israel na kamanda wa zamani wa jeshi la utawala huo, Benny Gantz, ametoa kauli kali dhidi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wakati wa mahojiano ya moja kwa moja kwenye Channel 12 ya Israel, akieleza hasira yake kufuatia taarifa za kuuawa kwa wanajeshi wa Israel katika mapigano kusini mwa Lebanon.
Gantz alisema kuwa badala ya kumwita Netanyahu kwa jina lake, anapaswa kuitwa "punda", akimlaumu kwa kushindwa kushughulikia hali ya usalama inayozidi kuzorota.
Aliongeza kuwa wanajeshi wa Israel wanaendelea kuuawa katika maeneo mbalimbali ya kusini mwa Lebanon, huku akiwashutumu baadhi ya wanasiasa na wafuasi wa Netanyahu kwa kupuuza hali halisi kutokana na uungaji mkono wao wa kisiasa.
Aidha, Gantz alionya kuwa Israel ipo katika hatari ya kusambaratika ikiwa uongozi wa sasa utaendelea na sera zake, akisisitiza kuwa mgawanyiko wa ndani na changamoto za kiusalama vinaendelea kuongezeka.
Your Comment